HOME

Apr 18, 2012

EXCLUSIVE:NAIBU WAZIRI NYALANDU AKANUSHA TAARIFA ZA KUTISHIA KWA BASTOLA!!

Naibu waziri wa viwanda na biashara amekanusha taarifa za kutishia
kwa bastola na kuwashutumu baadhi ya viongozi waandamizi wa chama cha mapinduzi CCM kuhusika na mpango wa kumchafua kisiasa.


Akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari katika viwanja vya bunge mjini Dodoma Waziri  Nyalandu amesema ameshtushwa na taarifa hizo ambazo zimeandikwa na vyombo mbalimbali vya habari kwa kile alichodai kuwa ni njama zinazofanywa na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM Mkoani Singida.


Amesema taarifa za yeye kutishia kwa bastola amezisikia akiwa katika shughuli zake za kiserikali Bungeni Mjini Dodoma na kwamba hakuwepo katika eneo la tukio licha ya ukweli kuwa wasaidizi wake wamehusishwa kwa kutoa kamba ya kizuizi cha barabarani ambacho hakikuwa na ulinzi wowote nyakati za usiku wa saa sita na si kutisha mtu ama kundi la watu kwa kutumia bastola.


Waziri Nyalandu amaesema licha ya kunyweshwa sumu mara mbili  na watu wasiomtakia mema hatasitisha nguvu na juhudi zake katika kulitumikia taifa kiuadilifu.

No comments:

Post a Comment