HOME

Apr 13, 2012

WANANCHI WAMETAKIWA KUZINGATIA TAHADHARI ZINAZOTOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA!!

Serikali imewataka wananchi kuzingatia tahadhari zote zinazotolewa na mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini ili kuepukana na matatizo ya uharibifu wa mali pamoja na maafa yanayoweza kuepukika katika kipindi cha tahadhari badala ya kupuuzia na kuanza kualalamika mara baada ya athari kutokea.

Hayo yamesemwaleo bungeni mjini Dodoma na naibu waziri wa uchukuzi mh Athumani Mfutakamba wakati akijibu swali la mh Mh David Silinde aliyetaka kufahamu ni kwanini kitengo cha masuala ya hali ya hewa nchini kinashindwa kutoa taarifa sahihi za hali ya hewa ambazo zingeweza kunusuru uharibifu wa mali pamoja na maafa yaliyotokea katika mikoa ya Dar es salaam na Mbeya.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa uchukuzi mh SILINDE amesema mamlaka ya hali ya hewa nchini inahitaji kupongezwa kwa kutoa taarifa sahihi za tahadhari kwa wananchi badala ya kulaumiwa huku tatizo kubwa likionekana kuwa kwa wananchi kutokana na kupuuza taarifa hizo.

No comments:

Post a Comment