Msanii wa maigizo ya filamu Elizabeth Michael mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Tabata leo amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka yanayomkabili ya mauaji ya msanii mwenzake wa maigizo Steven Charles Kanumba.
Mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ya mauaji.
Wakili alidai kwamba upelelezi haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena tarehe 23 mwezi wa nne mwaka huu.
Mshtakiwa aliletwa mahakamani hapo kwa siri akiwa kwenye gari lenye namba za usajiri T848BNV aina ya Isuzu ambayo pia ilikuwa na number nyingine za usajiri PT 2365 kwenye vioo.
Mshtakiwa alisindikizwa na askari wawili wa kike na mmoja wa kiume ambapo mshtakiwa alikuwa amevalia dila lenye rangi ya njano na mtandio wa pink na ndala nyekundu.
No comments:
Post a Comment