Ndege mpya ya Mswati III aina ya DC-9 twin-engine |
Mfalme Mswati wa tatu wa Swaziland |
Msemaji wa serikali nchini Swaziland amesema mfalme Mswati wa tatu nchini humo amepokea ndege mpya kama zawadi kutoka kwa wahisani ambao hawajatajwa.
Msemaji huyo Percy Simelane amesema ndege hiyo aina ya DC-9 twin-engine ni kwa matumizi ya mfalme khuyo na wake zake 13.
Chama cha nchini Swaziland kilichopigwa marufuku kimesema kuwa fedha za walipa kodi zinaweza kuwa zimetumika kununua ndege hiyo lakini Simelane amekanusha taarifa hiyo.
Mwaka 2002 mfalme huyo alijaribu kutumia fedha za umma kufanya manunuzi ya ndege hiyo lakini manunuzi hayo yalisitishwa baada ya maandamano ya mitaani.
No comments:
Post a Comment