Watu wanne wamekufa mapema leo katika makazi duni ya Mathare jijini Nairobi nchini Kenya baada ya kuangukiwa na kifusi kufuatia maporomoko ya ardhi.
Ajali hiyo mbaya imetokea mapema alfajiri baada ya jiwe kubwa kuporomoka kutoka kilimani huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha na kuangukia katika makazi hayo.
Kamishna mkuu wa Polisi Mathew Iteere amethibitisha vifo vya watu hao akiwa katika eneo la tukio ambapo watu wanane wamekimbizwa Hospitali ya taifa ya Kenyata kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment