HOME

Apr 13, 2012

SERIKALI KUNUNUA RADA NYINGINE KUIMARISHA UTABIRI WA HALI YA HEWA!!

Katika kuimarisha shughuli za utabiri wa hali ya hewa nchini Serikali imeshanunua rada moja ambayo iko jijini Dar es Salaam huku ikiwa mbioni kununua rada nyingine ambayo itapelekwa jijini Mwanza ikiwa ni jitihada za kuiwezesha mamlaka hiyo kutoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa usahihi zaidi.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa uchukuzi Mh. Athumani Mfutakamba wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum Mh Maua Daftari aliyetaka kufahamu mpango wa serikali wa kununua rada kwa ajili ya kuiboresha mamlaka ya hali ya hewa
umefikia wapi.

Naibu waziri huyo amesema katika kuonesha kuwa TMA inatoa taarifa sahihi Tanzania imepokea zawadi kwa kutabiri vyema matukio mbalimbali yanayotokea nchini.

No comments:

Post a Comment