HOME

Apr 30, 2012

MATUKIO RASMI KILI 2012 WINNERS TOUR NDANI YA DODOMA!!!!


Mshindi wa pili aliyepatikana katika msako wa vipaji vipya vitakavyopanda Jukwaani na washindi wa tuzo za Kili akitoa burudani
Mshindi wa kwanza aliyepatikana katika msako wa vipaji vipya vitakavyopanda Jukwaani na washindi wa tuzo za Kili akitoa burudani
Washindi wa ziara ya kusaka vipaji vipya vitakavyopanda jukwaani na washindi wa tuzo za Kili.
Mshindi wa Tatu waliopatikana katika ziara ya kusaka vipaji vipya vitakavyopanda jukwaani na washindi wa tuzo za Kili akionyesha ukali wake.
Watu kibao wakazi wa Dodoma waliojitokea kuburudika na wasanii wao wanaowapenda
Mmoja wa Ma MC Dula ''Mjukuu wa Ambua''
Ma MC wa siku hiyo Dula na Sam Misago kutoka East Africa Radio
Kwenye mashine alikuwa Dj kutoka East Africa Radio Dj Kim
Ben Pol akifanya vitu vyake
Barnaba nae alikuwepo kwasha moto wa Kili Tour
Msanii AT nae hakubaki nyuma kuwapa burudani mashabiki wake
Diamond akishambulia Jukwaa
Roma akiingia kwa Steji
Mwanamuziki bora wa Hip Hip Hop aliyetoa shoo bora ya Hip Hop Roma Mkatoliki
Ommy Dimpoz na Dancers wake


Alli Kiba akitoa burudani

Apr 27, 2012

PEP GUARDIOLA ATANGAZA KUJITOA BARCELONA!!

Pep Guardiola inasemekana ameuambia uongozi wa klabu ya Barcelona kuwa hataendelea kuinoa timu hiyo mara baada ya msimu huu kumalizika.

Guardiola ambaye aliwahi kuicheza klabu hiyo kabla ya kuwa kocha wa kikosi cha pili na hatimaye kikosi cha kwanza anatarajia kutangaza uamuzi wake huo atakapokuwa na mkutano na waandshi wa habari.

Wakati huo huo nahodha wa Chelsea John Terry ataruhusiwa kulipokea kombe la klabu bingwa barani Ulaya ikiwa timu yake ya Chelsea itaifunga Bayern Munich katika fainali itakayopigwa Maei 19,UEFA imethibitisha kupitia BBC Sport.

ECOWAS KUPELEKA MAJESHI MALI NA GUINEA-BISSAU!!

Viongozi wa nchi za Afrika magharibi ECOWAS wamekubaliana kupeleka majeshi nchini Mali na Guinea-Bissau kufuatia mapinduzi ya kijeshi katika nchi hizo.


Umoja huo wa nchi za Afrika magharibi umesema kwamba baada ya mkutano wa dharura,viongozi hao wanatarajia kuona uchaguzi wa urais katika nchi hizo unafanyika katika kipindi cha miezi 12 ijayo.


Kati ya askari 500 na 600 watapelekwa nchini Guinea-Bissau haraka iwezekanavyo wakati askari 3,000 kutoka umoja huo wanatarajiwa kupelekwa nchini Mali kusaidia majeshi ya nchi hiyo kupambana na waasi ambao wanadhibiti eneo la kaskazini.

''THE AVENGERS'' KUINGIA SINEMA LEO!!

Katika kuangalia kwangu filamu za marvel ,The avengers-watazamaji hatutaweza subiri mpaka mwisho wa filamu kushangilia kwani katikati ya action sequence katika onyesho la tatu la story, team nzima ya avengers,ikijumuisha Iron man, Hulk, Thor,  Captain america, Hawkeye, na Black Widow, wana assemble kwenye screen na kufanya mtazamaji kubaki na butwaa.

Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani filamu hii livyo tengenezwa kwa umakini mkubwa na jinsi waigizaji wake wanavyoweza kusadifu uhusika wao na jinsi dialogue na script vilivyo tengenezwa kwa umakini pia.

Avenger ni muendelezo wa baadhi ya ya filamu za marvel universe. Filamu inaanza pale Loki (Tom hilddleston) anaporudi tena dunia na kuiba “the Tesseract” an alien source of pure energy, na kutishia kuteka dunia nzima kwa msaada wa jeshi lake la viumbe kutoka dunia nyingine liitwalo “the chitauri”.

Nick Fury (Samuel L. Jackson), kiongozi wa covert government outfit inayoitwa  S.H.I.E.L.D anaunda team ya super heroes iitwayo The Avengers (Robert Downey Jr,Chris Hemsworth, Chris Evans, Mark Ruffalo, Scarlett johnsson, Jeremy Renner)  kuzuia mipango ya Loki.

Kwa hisani ya Gonga Mx

Apr 26, 2012

ROMA KUTENGENEZA DOCUMENTARY YA MAISHA YAKE!!

Roma (kati) akiwa na Ma presener wakali kutoka EATV Lotus Kyamba (kushoto) wa kipindi cha Nirvana kila Jumanne saa moja usiku na Baby Drama Faiza wa 5Selekt kila siku za wiki Jumatatu mpaka Ijumaa saa @1500 -1700hrs.
Msanii anayeng'ara katika anga za muziki nchini Tanzania na kuwakilisha mkoa wa  Tanga Roma mkatoliki ameweka bayana kuwa,baada ya kuchukua tuzo mbili za muziki za Kilimanjaro Music Awards hivi karibuni kama Msanii bora wa Hip Hop na wimbo wake Mathematics kuchukua kama wimbo bora wa Hip Hop hivi sasa anatengeneza Documentary yake inayoeleza maisha yake kimuziki toka alivyoanza mziki shida alizopitia mpaka kufikia hivi sasa alipofikia. 

Roma ambae pia utamshuhudia katika Kili Tour inayoanza Jumamosi mkoani Dodoma na kuzunguka katika mikoa kadhaa akiwa pamoja na wakali wengine wa muziki Tanzania walioshinda tuzo hizo amefunguka kuwa ni mapema sana kusema itatoka lini ila haitochelewa kutokana kuwa anaamini watu wataipenda na italeta utofauti kidogo maana story iliyomo ndani ya Documentary hiyo iko kitofauti na itamgusa kila mmoja.

WACHEZA BASKETBALL TIMU YA ANDY 1 NDANI YA EAST AFRICA RADIO LEO MCHANA!!

Wacheza mpira wa kikapu timu ya Andy 1 ambao wako Bongo kwa sasa leo walipata nafasi ya kutembelea studio za East Africa Radio na kufanya interview katika kipindi cha Power Jams na Sam Misago,Anna Peter na Dj AD ambaye jana alisherekea siku yake ya kuzaliwa.

MFALME MSWATI III APOKEA NDEGE MPYA!!

Ndege mpya ya Mswati III aina ya DC-9 twin-engine
Mfalme Mswati wa tatu wa Swaziland
Msemaji wa serikali nchini Swaziland amesema mfalme Mswati wa tatu nchini  humo amepokea ndege mpya kama zawadi kutoka kwa wahisani ambao hawajatajwa.

Msemaji huyo Percy Simelane amesema ndege hiyo aina ya  DC-9 twin-engine ni kwa matumizi ya mfalme khuyo na wake zake 13.

Chama cha nchini Swaziland kilichopigwa marufuku kimesema kuwa fedha za walipa kodi zinaweza kuwa zimetumika kununua ndege hiyo lakini Simelane amekanusha taarifa hiyo.

Mwaka 2002 mfalme huyo alijaribu kutumia fedha za umma kufanya manunuzi ya ndege hiyo lakini manunuzi hayo yalisitishwa baada ya maandamano ya mitaani.

CHARLES TAYLOR AKUTWA NA HATIA!!

Majaji katika mahakama maalum ya kimataifa wamempata na hatia Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor na hatia ya kufadhili vita nchini Sierra Leone.

Taylor ameshtakiwa mbele ya mahakama maalum inayochunguza uhalifu wa kibinadamu nchini Sierra Leone.

Kesi dhidi ya kiongozi huyu imechukua takriban miaka mitano.

Taylor alituhumiwa kwa kuwaunga mkono waasi ambao waliwaua maelfu ya raia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone kati ya mwaka 1991-2002.

Jaji mwandamizi wa kesi ya Charles Taylor Richard Lussick amesema mahakama inao ushahidi kwamba Taylor alifadhili kwa hali na mali maasi ya nchi jirani ya Sierra Leone.

WAZIRI AKIRI KUNUNUA NYUMBA YA MAMILIONI!!

Siku chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti taarifa za uchunguzi kwamba kuna mawaziri wawili ambao wamenunua nyumba mbili zenye thamani ya Sh1.8 bilioni, mmoja wa mawaziri hao, Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii ameibuka na kukiri.Maige aliliambia gazeti hili jana kuwa nyumba yake hiyo iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam, ameinunua kwa Dola za Marekani 410,000 (takriban Sh656 milioni) ambazo anadai kuwa ni mkopo kutoka Benki ya CRDB.

Hata hivyo, wakati Waziri Maige akieleza kuwa nyumba hiyo ina thamani hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli amedai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba ilinunuliwa kwa fedha taslimu Dola 700,000 za Marekani (takriban Sh1.1 bilioni).

Awali, habari zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa Waziri Maige alinunua nyumba hiyo kutoka kwa Kampuni ya Savana Real Estate.

Mmoja wa madalali wanaouza nyumba za kampuni hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Athuman (Ustadhi) alilithibitishia gazeti hili kwamba Waziri Maige amenunua nyumba moja kati ya nne zilizoko sokoni.
Habari na Picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi zaidi INGIA HUMU.

HAPPY MUUNGANO DAY 26 APRIL...MUNGU UBARIKI MUUNGANO WETU!!

HAPPY BIRTHDAY DJ AD ''MAFUVU BEEIBY'' WA EAST AFRICA RADIO 25 APRIL...MAY GOD BLESS YOU BROTHER!!


Siku ya Jana tarehe 25 April ilikuwa siku ya kuzaliwa ya rafiki na Dj Mahiri kutoka East Africa Radio wengi tunamfahamu kwa jina la Dj AD au Mafuvu Beeiby au The TurntableList kama anavyopenda kujiita.Hapo akiwa na keki yake muda mfupi baada ya kuletwa,Mungu akuzidishie kaka maisha marefu na heri katika kazi zako.
Mimi kulia pamoja na AD na dada yetu wa Reception ITV Da Naima
Mimi na AD.

TAHADHARI YA MAFURIKO YATOLEWA KENYA!!

Serikali ya Kenya imeonya wakazi wake wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhama mara moja ili kujiepusha na mafuriko.


Katibu mkuu wa wizara ya programu maalum nchini Kenya  Bw. Andrew Mondoh ametoa taarifa ya tahadhari kwa maeneo ya Budalangi, Kano, Wareng Pokot, Baringo , Pwani na baadhi ya maeneo ya Nairobi kuwa maeneo makuu yanayoweza kuathiriwa na mafuriko katika siku sita zijazo.


Tahadhari hiyo inakuja kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zilizosababisha mafuriko katika maeneo kadhaa ambapo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu 36 na kuharibu mali.

HUKUMU YA TAYLOR KUTOLEWA LEO!!

Majaji katika mahakama maalum kuhusu vita nchini Sierra Leone, leo wanatarajia kutoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor kwa kuhusika na vita hivyo vilivyodumu miaka 10.


Bw. Taylor anakabiliwa na mashtaka 11 ikiwemo ubakaji na mauaji ya raia wa Sierra Leone na ikiwa atapatikana na hatia atakuwa rais mstaafu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa.


Zaidi ya mashaidi 100 wamefika mbele ya mahakama hiyo lakini Bw Taylor amekanusha kuhusika na uhalifu huo wakivita na anadai kuwa kesi hiyo ni njama ya kummaliza kisiasa.


Inakadiriwa kuwa zaidi wa watu elfu 50 waliuawa na wengine wakiwemo wanawake na watoto walibakwa na kukatwa mikono au miguu na waasi wa RUF ambao upande wa mashtaka unasema walipata usaidizi wa silaha kutoka kwa Bw Taylor.

WAWILI WAFARIKI DUNIA KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI MKOANI SONGEA!!

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti wilayani Songea mkoani Ruvuma likiwemo la mtoto mwenye umri wa miaka miwili kufariki baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji huku mmoja mwenye umri wa miaka themanini akifariki dunia baada ya kugongwa na gari ambalo halikuweza kufahamika mara moja.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda ni kuwa tukio la kwanza la mtembea kwa miguu Kanisia Nyoni(80) kugongwa na gari na kufariki dunia papo hapo lilitokea katika eneo la kata ya Tanga nje kidogo ya mji wa Songea.


Amesema kuwa mtu huyo alipatwa na ajali hiyo katika bara bara ya Songea-Makanbako ambapo gari lililokuwa katika mwendo kasi majira ya saa moja usiku lilimgonga Bi. kizee huyo aliyekuwa akirejea nyumbani kwake na jeshi la polisi mkoani Ruvuma linaendelea kufanya uchunguzi ili kulibaini gari hilo lililohusika katika ajali hiyo.

RAIS WA MPITO MALI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI!!

Rais wa mpito Diouncounda Traore,
Rais wa serikali ya mpito wa Mali ametangaza serikali mpya,kwa kuwapa madaraka wanajeshi.


Wawakilishi wa majeshi wamepewa nyadhifa za Wizara ya Ulinzi, Wizara ya usalama wa nchini na masuala ya nchini.


Askari waliipindua serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasi takriban mwezi mmoja uliopita.


Viongozi wa mapinduzi hayo baadaye waliamua kukabidhi madaraka kwa Rais wa mpito Diouncounda Traore, aliyewajibishwa kuona kua ratiba ya uchaguzi inapangwa na kutekelezwa.


Mpango huu ulifikiwa na Shirikisho la kimkoa la Ecowas ambalo lilitaka kuhakikisha kwamba madaraka yarejeshwe kwa serikali itakayochaguliwa kwa kura.

Apr 25, 2012

WANAWAKE UGANDA WAANDAMANA VIFUA WAZI!!

Jeshi la polisi nchini Uganda limeanzisha upelelezi wa ndani ya jeshi hilo kwa maafisa wake ambao walihusika na tukio la kumkamata kiongozi wa wanawake wa chama cha FDC Ingrid Turinawe Ijumaa iliyopita kwa tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia.


Kiongozi huyo amedaiwa kufinywa matiti yake na kuwekwa wazi na maafisa wa polisi ambao walimtia mikononi wakati akielekea katika mkutano wa vyama vya upinzani huko Nansana.


Kundi la wanawake nchini Uganda wamevua nguo na kubaki vifua wazi wakilalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kijinsia mwanasiasa wa upinzani Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.


Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo.

Apr 24, 2012

NORTH KOREA'S NUCLEAR TEST READY!!

North Korea has almost completed preparations for a third nuclear test, a senior source with close ties to Pyongyang and Beijing told Reuters, which will draw further international condemnation following a failed rocket launch if it goes ahead.


The isolated and impoverished state sacrificed the chance of closer ties with the United States when it launched the long-range rocket on April 13 and was censured by the U.N. Security Council, including the North's sole major ally, China.


Critics say the rocket launch was aimed at honing the North's ability to develop an intercontinental ballistic missile capable of hitting the United States, a move that would dramatically increase its military and diplomatic heft.


Now the North appears to be about to carry out a third nuclear test after two in 2006 and 2009.

CUF YATOA MSIMAMO SAKATA TANDAHIMBA!!

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchu – CUF Taifa Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam
MSIMAMO WA CHAMA


-Serikali haitakwepa kuwajibika kwa hasara zilizojitokeza na watu walioumizwa katika tukio hilo.


-Serikali iwalipe wafanyabiashara wote kwa mali walizopoteza na majengo yaliyoharibiwa.


-Serikali iwalipe fidia watu wote walioumizwa kwa risasi au vipigo vya polisi katika operesheni hiyo ya kikatili ya polisi dhidi ya wananchi.


-Serikali iwafute kazi na iwafikishe mahakamani viongozi wote wa polisi na askari waliohusika na matukio hayo.


-Serikali imfukuze kazi mkuu wa wilaya ya Tandahimba ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa kushindwa kuongoza na kuwaeleza wananchi wa Tandahimba namna serikali inavyoshughulikia tatizo la malipo yao ya pili ya korosho.


-Vitendo walivyofanya polisi Tandahimba vinajenga uhasama mkubwa kati ya raia na jeshi la polisi. Serikali iunde tume huru maalum ya uchunguzi na ambayo haitawahusisha polisi ili ikafanye uchunguzi wa kina na wa wazi na kisha tume hiyo itangaze hadharani mambo iliyoyabaini na kuishauri serikali hatua za kuchukua ili kuondoa uwezekano wa vitendo hivyo vya kimakusudi na kikatili kujirudia mahali pengine ndani ya Tanzania.


-Tume ya Haki za binadamu ifanye uchunguzi wake kubaini uvunjifu wa haki za binadamu Tandahimba na kuwawajibisha wahusika na kupendekeza hatua za kuchukua hali hiyo isirudiwe Tandahimba na kokote Tanzania.


-Asasi za kiraia za haki za binadam na Msaada wa Kisheria wawape msaada wa kisheria wahanga na waathirika wa Tandahimba waweze kudai haki zao.


-Wakulima wapewe haki na uhuru wa kiuchumi wa kuuza korosho zao na mazao mengine kwa yeyote atakayewapa bei nzuri. Serikali iweke mazingira ya wafanya biashara kushindana kwa kuwapa bei nzuri wakulima  wa korosho na mazao mengine.

VIFO VYA GHAFLA VIMEAMSHA HISIA MPYA NCHINI SYRIA!!

Kuongezeka ghafla kwa idadi ya vifo nchini Syria kumeibua mashaka juu ya uwezekano wa kufanikisha mpango wa amani wa umoja wa mataifa wa kusitisha mapigano.


Wanaharakati wamesema watu 70 waliuwawa jana wengi katika maeneo ambayo yamekuwa yakishambuliwa na majeshi ya serikali katika mji wa Hama.


Serikali ya Marekani imesema timu ya uangalizi ya umoja wa mataifa iliyoko nchini Syria iko katika hatari kubwa ambapo umoja wa mataifa unasukuma kuongeza idadi ya waangaliaji,na mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa  Kofi Annan anatarajiwa kulipa taarifa baraza la usalama la umoja wa mataifa leo.

SOUTH SUDAN PRESIDENT VISITS CHINA FOR TALKS!!

South Sudan's president is visiting Beijing for talks with Chinese leaders, while the United Nations Security Council is scheduled to hold a closed-door session on the conflict between Sudan and South Sudan.


President Salva Kiir is due to meet Tuesday with Chinese President Hu Jintao. During his visit he will also open a new embassy for South Sudan in China.


The U.S., China, and other world powers have called on Sudan and South Sudan to stop fighting and resume peace talks.


Sudan's president, Omar al-Bashir, said Monday there will be no further talks and that the south only understands the language of “guns and ammunition.”

HUKUMU YA TAYLOR KUTOLEWA ALHAMIS!!

Aliyewahi kuwa rais wa Liberia Charles Taylor
Hukumu ya aliyewahi kuwa rais wa Liberia Charles Taylor inatarajiwa kutolewa siku ya Alhamisi kufuatia mashitaka yanayomkabili ya kuwapa silaha waasi wa Sierra Leone ili apate madini ya almasi katika miaka ya 90.


Jopo la majaji watatu linatarajiwa kusoma hukumu hiyo ya kihistoria, ambayo ni ya kwanza dhidi ya kiongozi wa zamani wa nchi kuwahi kutolewa na mahakama ya kimataifa, katika mahakama maalum kuhusu Sierra Leone mjini Leidschendam nje ya The Hague.


Taylor mwenye umri wa miaka 64, anatuhumiwa kwa kuwasaidia waasi wa kundi la Revolutionary United Front – RUF la Sierra Leone, kufanya mashambulizi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilisababisha vifo vya watu 120,000 kati ya mwaka wa 1991 na 2001.


Katika kesi hiyo iliyokamilika mwezi Machi 2011, mwanamitindo maarifu duniani Naomi Campbell alitoa ushahidi jinsi alivyopokea almasi kutoka kwa Taylor.

MACHAFUKO SUDAN YAZIDISHA HOFU YA VITA!!

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameshutumu mashambulio ya angani yanayofanywa na Sudan katika mipaka ya Sudan Kusini, na akiwataka viongozi wa nchi hizo mbili kuwacha kujiingiza katika vita.


Bw. Moon ameitaka Sudan isitishe mashambulio mara moja akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili.


Siku ya Jumatatu ndege za kijeshi za Sudan zilishambulia mji wa
Bentiu ulioko Sudan kusini na kusababisha maafa kwa raia wa kawaida na hasara kubwa katika mji huo.


Awali, Rais wa Bw. Sudan Omar al-Bashir alipuuza uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa na wanajeshi wake ndani ya Sudan Kusini.

HUDSON ATOA USHAHIDI MAHAKAMANI!!

Jennifer Hudson
Mwanamuziki Jennifer Hudson amepata wakati mgumu mahakamani hasa baada ya kushindwa kujizuia na kumwaga chozi  wakati alipokuwa akitoa ushahidi wake katika kesi inayoendelea ikimkabili aliyekuwa mume wa dada yake William Balfour kwa kuhusika na kuwaua wanafamilia yake watatu.


Hudson aliangia kilio hicho baada ya mwendesha mashtaka kumuuliza ni lini mara ya mwisho kuonana na ndugu zake hao na hasa pale alipoonyeshwa picha ya mama yake wakati akitoa maelezo ya ushahidi wake  jambo ambalo limegusa hisia za wengi.


Hudson katika ushahidi wake aliweka wazi kuwa, tangua awali hakuna hata mmoja wa wanafamilia yake aliyekuwa ameridhia swala la dada yake kujiingiza katika mahusiano na mtuhumiwa huyo wa mauaji William Balfour kutokana na kumuona kuwa ni mtu aliyekuwa na tabia za ajabu.