Tanzania imetakiwa kuwa makini na kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchi za jirani, ambao huingia nchini na kununua mazao kwa njia za magendo na baadaye kwenda kuuza nchi za nje huku wakijinadi kuwa kuwa mazao na bidhaa hizo zimetoka katika nchi zao.
Mwakilishi mkazi wa mtandao unaojishughulisha na ukuzaji uchumi na mauzo ya bidhaa nje ya nchi wa Trade Africa Network Tanzania Bw. Deusdedit Kizito, akizungumza leo jijini Dar es Salaam |
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakitekeleza majukumu yao. |
Mwakilishi mkazi wa mtandao huo Bw. Deusdedit Kizito, amesema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiinyima Tanzania fursa ya kunufaika na masoko ya kimataifa.
Katika kukabiliana na hali hiyo, Deusdedit ameishauri serikali kuhakikisha inatunga sera na sheria ya matumizi bora ya ardhi, ambayo pamoja na mambo mengine, itasaidia kuepusha utoroshwaji wa mazao lakini pia itatenganisha kati ya kilimo hai na kile cha kisasa.
No comments:
Post a Comment