HOME

Apr 22, 2013

MHE. LISSU AFUNGUKA...ATUMIWA MAELFU YA SMS!!

Mhe. Tundu Lissu (Laft), Joshua Nassari na Naibu Spika wa bunge Mhe. Job Ndugai nje ya ukumbi wa bunge.
Mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Mhe. Tundu Lissu leo ameamua kufunguka na kusema kuwa kiti cha spika hakikuwatendea haki baada ya yeye na wenzake watano kutolewa nje ya ukumbi wa bunge na kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya bunge.

Mhe. Lissu amesema kuwa adhabu hiyo haipo kikakuni kama ilivyodaiwa na kwamba imefanywa si kwa maamuzi ya spika au kanuni bali ni kwa shinikizo kutoka upande fulani.

Akizungumza leo asubuhi, Mbunge huyo wa Singida Mashariki kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA amesema baada ya tukio hilo alipokea maelfu ya jumbe za simu kutoka kwa wananchi ambapo amesema ni vyema wakatulia kwani hawezi kumjibu kila mmoja.

Mhe. Lissu amefafanua kuwa ni ushamba kwa watu kuona ni kitu cha ajabu kushangaa wanachokifanya bungeni kwakuwa kimekuwa kikifanywa pia mabunge makubwa makubwa akitolea mfano mabunge ya nchi za nje ambayo hufikia hatua ya kurushiana viti na kusema wao wako pale kutetea maslahi ya wananchi na si vinginevyo.

Mfano wa kile ambacho wakati mwingine hutokea kwenye mabunge ya nchi za nje, Hilo ni bunge la Ukraine hapo waheshimiwa walishindwa kuelewana kidogo na hicho ndio kilichotokea.
Akizungumzia anachokifanya sasa wakati akiwa nje ya bunge, Mhe Lissu amesema anaendelea na shughuli za kitaifa kama kawaida ambapo kwa sasa yuko jijini Dar es salaam akitekeleza majukumu yake ya kichama na taifa kwa ujumla hivyo watanzania wasiwe na wasiwasi.




No comments:

Post a Comment