HOME

Apr 18, 2013

EXCLUSIVE PHOTOS:CHILLAH AMLILIA BI. KIDUDE, AMSUBIRISHA "BEAUTIFUL"!!

Star Muziki nchini Tanzania Aboubakar Shaban Katwila maarufu kama Q Chief amezungumza na blog hii na kuweka wazi jinsi alivyoguswa na kusikitishwa sana na kifo cha nguli wa muziki nchini Tanzania Bi Kidude aliyefariki dunia jana mchana mazishi yake kufanyika leo.

Chillah amesema msiba huo mkubwa sana kwake umemfanya hata achelewe kurelease ngoma yake mpya pamoja na video, ngoma inayokwenda kwa jina la Beautiful.

Amesema ''Natarajia kuachia wimbo wangu mpya uitwao beautiful, Nimeshalipia video yake mapema baada ya maombolezo ya nguli wa muziki wa taarab nchini Bi Kidude Mungu amuafu na kumpa wepesi. Nimelazimika kuchelewesha ku release na kuanza ku shoot kutokana na msiba. Mashabiki wategemee kitu tofauti kutoka kwa Chillah tofauti ya wimbo huu utakuwa ni zawadi ya pekee kwa mashabiki wangu na nitasherekea siku yangu ya kuzaliwa kwa aina ya pekee nawaomba watanzania wanisubiri kiduchu Nawapenda sana.''

No comments:

Post a Comment