HOME

Apr 18, 2013

WABUNGE 5 KUTOLEWA NJE YA BUNGE,SPIKA MAKINDA KUTOA MAELEZO!!

Spika wa bunge la Tanzania Mhe. Anna Makinda amesema kuwa atatoa ufafanuzi kuhusu hali ya sintofahamu iliyotokea jana katika bunge la Tanzania baada ya wabunge watano wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kutolewa nje na kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge kwa siku tano.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa upinzani kupitia kwa kiongozi wa kambi hiyo Mhe. Freeman Mbowe kuomba mwongozo wa spika leo bungeni mjini Dododma kuhusiana na hatua hiyo iliyochukuliwa na naibu spika wa bunge Job Ndugai ambayo amesema imezua maswali miongoni mwa wabunge.

Spika Makinda amewata wabunge kuwa watulivu na kuacha malumbano kwani atatoa ufafanuzi wa jambo hilo katika vikao vya jioni vya bunge.

Wabunge waliokumbana na kadhia hiyo ya kutolewa nje ya ukumbi wa bunge ni Mbunge wa Nyamagana Hezekiah Wenje, Highness Kiwia wa Ilemela, Joseph Mbilinyi wa Mbeya Mjini, Godbless Lema wa Arusha mjini na Mchungaji Peter Msigwa wa Iringa Mjini ambapo chanzo cha kufukuzwa kwao kimedaiwa ni kuwazuia askari wa bunge kumtoa nje Lissu ambaye alikuwa ameamriwa kutoka nje na naibu Spika baada ya kuingia hotuba ya Mwigulu Nchemba mbunge wa Iramba Mashariki.

No comments:

Post a Comment