HOME

Apr 22, 2013

TETEMEKO BAYA LAUA CHINA!!

Vikosi vya uokoaji nchini China vimefanikiwa kufika kwenye vijiji vya mbali milimani vilioko Kusini-magharibi mwa nchi hiyo katika jimbo la Sichuan lililokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi.

Waokoaji hao wamekuwa safarini kwa miguu kufikia vjiji hivyo
kutokana na kutokana na ugumu wa barabara na maporomoko katika maeneo hayo ya mbali.

Mawasiliano bado yameharibiwa hivyo kiwango cha uharibifu kamili bado hakijajulikana.

Vyombo vya habari vya nchi hiy vimeripoti kuwa watu 207 wamefariki dunia au wamepotea kutokana na tetemeko hilo ambapo watu elfu 11 na 500 wamejeruhiwa huku 960 wakiwa na hali mbaya zaidi.

No comments:

Post a Comment