HOME

Apr 22, 2013

FULL VIDEO:LUIS SUAREZ ALIVYOMNG'ATA IVANOVIC!!

Mshambuliaji wa timu ya Liverpool Luis Suarez anaweza kujikuta matatizoni na chama cha soka England baada ya kumng'ata beki wa kati wa Chelsea Branislav Ivanovic katika pambano la Ligi kuu England katika uwanja wa Anfield jana usiku.

Pambano hilo lilimalizika kwa sare ya bao 2 - 2 ambapo Liverpool walikuwa nyuma wakati tukio hilo linatokea huku tayari akiwa amesababisha penalti, Suarez alionekana ameng'ang'ania mkono wa Ivanovic na kumng'ata kwa nguvu.

Suarez ameshaomba radhi kutokana na tukio hilo ambapo chama cha soka England leo kinatarajiwa kuongea.


No comments:

Post a Comment