Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lite iliandaa hafla maalum ya maafisa masoko '' Marketer's Night Out iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip siku ya Alhamis na kuhudhuriwa na maafisa masoko kutoka makampuni mbalimbali ambapo msemaji mkuu alikuwa Dk. Wale Akinyemi kutoka Nigeria ambaye alitoa mafunzo muhimu sana kwa ustawi wa makampuni mengi hapa nchini.
Hawa ni warembo ambao walihusika katika kukaribisha wageni waliofika katika hafla hiyo iliyofana sana pale Golden Tulip. |
Maafisa masoko kutoka makampuni mbalimbali wakiwa wamejumuika katika picha ya pamoja na Msemaji mkuu katika hafla hiyo ya Marketer's night out Dk. Wale Akinyemi kutoka Nigeria. |
Msemaji mkuu katika hafla hiyo ya Marketer's night out Dk. Wale Akinyemi kutoka Nigeria akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya bia Serengeti kupitia kinywaji cha Tusker Lite. |
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti Steve Gannon akiwakaribisha wageni waalikwa katika hafla hiyo kubwa na nzuri ambayo hufanyika mara kwa mara ya Marketer's night Out. |
Mkurugenzi wa masoko wa SBL Mr. Ephrahim Mafuru akizungumza machache katika hafla hiyo |
Katika hafla hiyo kulikuwa na vyakula vya kila aina kukamilisha shughuli nzima ambapo watu walisevia vya kutosha tu. |
Watu walipata misosi ya nguvu na kushushia na kinywaji rasmi cha usiku huo Tusker Lite |
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo. |
Wafanyakazi wa EATV kutoka upande wa Marketing wakiwa katika hafla ya Marketer's night out iliyofanyika katika hoteli ya Golden Tulip. |
Wageni kutoka makampuni mbalimbali kulia ni mtangazaji wa kipindi cha Nirvana Deogratius Joseph Kithama na Ziada Abeid kutoka Push Mobile pamoja na rafiki. |
B Band wakiongozwa na Banana Zorro ndio walikuwa watumbuizaji wakuu katika haflya hiyo ambapo waliporomosha burudani nzuri unaweza kujionea mwenyewe katika picha jinsi Dancing Floor ilivyosheheni. |
No comments:
Post a Comment