Mkurugenzi wa rasilimali watu katika jeshi la polisi nchini Uganda Charles Birungi amesema kuwa jeshi la nchi hiyo lipo tayari katika kukabiliana na shambulizi lolote la kigaidi kama lililotokea Julai 2010.
Bw. Birungi amesema kuwa pia jeshi la polisi linaendelea na mchakato wa kujiweka tayari kupambana na shambulio lolote la kigaidi.
Ameweka wazi kuwa mashambulizi yoyote ya baadae katika nchi hiyo yatakabiliwa kwa kutumia teknologia na wanajeshi waliopatiwa mafunzo vizuri.
No comments:
Post a Comment