HOME

Apr 19, 2013

VOICE: WASIOSAJILI SIMU FAINI AU KWENDA JELA!!

Mkurugenzi wa TCRA, Prof. John Nkoma.
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kwa wananchi ambao wanatumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa kuwa ni kosa la jinai kwani adhabu yake ni kifungo cha miezi mitatu gerezani ama faini ya shilingi laki tatu za kitanzania.

Mamlaka hiyo ikishirikiana na makampuni ya simu imetangaza kuzifunga namba za simu ambazo hazijasajiliwa ili kuwalinda watumiaji kwa ajili ya kuimarisha usalama.

Akiongea jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA, Prof. John Nkoma amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kubaini ukiukwaji mkubwa wa matakwa wa sheria licha ya usajili wa namba za simu kuwa wa lazima kwa mujibu wa sheria ya Mawasiliano ya kielektroniki na Posta, EPOCA ya mwaka 2010.

Prof. Nkoma amesema watumiaji,watoa huduma wakala wa makampuni ya simu za mkononi na wananchi wanakumbushwa kwamba ni kosa kisheria kutumia au kuwezesha kutumiwa kwa namaba ya simu ambayo haijasajiliwa.

Msikilize Prof. Nkoma akifafanua zaidi hapa....


No comments:

Post a Comment