Taarifa zilizofikia blog hii hivi punde zinahabarisha kuwa mkongwe wa muziki wa taarab nchini Tanzania, Kidude Binti Baraka maarufu Bi Kidude amefariki dunia.
Inasemekana, Bi. Kidude ambaye ametamba na nyimbo nyingi sana zilizomfanya atambulike kitaifa na kimataifa na kuiwakilisha vyema Tanzania alikuwa akiugua kwa muda mrefu hadi umauti unamkuta.
Mungu ailaze Pema peponi roho ya marehemu Kidude Binti Baraka. Amin.
Taarifa zaidi endelea kufuatilia hapa tutakujuza zaidi. RIP Mpendwa wetu.
No comments:
Post a Comment