Picha ya washukiwa wawili wa shambulio la Boston Marathon karibu kabisa na eneo la tukio. |
Shirika la Upelelezi la FBI limetoa picha za watuhumiwa wawili wanaotaka kuwatambua kama sehemu ya uchunguzi wao kuhusiana na mashambulizi ya siku ya Jumatatu ya Boston Marathon.
Kamera za CCTV zilifanikiwa kunasa wanaume wawili waliokuwa
wamevalia kofia nyeusi na mwingine nyeupe karibu kabisa na eneo
lilipotokea tukio hilo.
Afisa wa FBI Richard DesLauriers amewaonya wananchi kutowakaribia wanaume hao wawili.
Hapo awali katika kuwakumbuka waliokufa katika mashambulizi hayo,rais Barack Obama wa Marekani aliahidi kuwapata waliohusika na
tukio hilo.
Video ya sekunde 30 iliyotolewa na FBI ikimwonyesha mshukiwa akitembea mitaani karibu kabisa na eneo la tukio.
Video ya sekunde 30 iliyotolewa na FBI ikimwonyesha mshukiwa akitembea mitaani karibu kabisa na eneo la tukio.
No comments:
Post a Comment