HOME

Apr 22, 2013

"NOTHING BUT THE TRUTH" YA JIDE KUTOKA MEI 31!!

Star wa Muziki nchini Tanzania Komandoo Lady Jay Dee anatarajia kuachia albamu yake mpya Tarehe 31 Mei mwaka huu, Albam aliyoipa jina la ''Nothing but the truth''.

Jide ambaye kwa sasa anatamba na kipindi chake bora kabisa cha Diary ya maisha yake '' Diary ya Lady Jay Dee'' kinachorushwa EATV kila siku ya Jumapili saa tatu kamili usiku amesem taarifa kamili za jinsi gani albam hiyo itakuwepo eneo la karibu na wewe mteja itatolewa siku ya Jumatano.

Pia amefunguka kuwa tarehe ya Show ya miaka 13 ya LADY JAYDEE itatangazwa baadae kila kitu kikiwa tayari na kuwaomba mashabiki kumpa support kubwa.

''Kuna fitna kubwa imepagwa, wafitini wanasubiri tutangaze tarehe yetu tu na wao watangaze tarehe hiyo hiyo sawa na yetu, Na tena wachague venue ya jirani na tutakapofanyia sisi show.'' Jide alifunguka

Chini ni List ya nyimbo ambazo zitakuwepo ndani ya Albamu hiyo.

1. Joto Hasira
2. Yahaya
3. Njiwa
4. Nimekusamehe
5. Historia
6. Tell Him
7. When You Cry
8. Why?
9. Msichoke Feat: Machozi Band
10. Yeye (Bonus Track)

No comments:

Post a Comment