Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa, Takriban watu 16 wamefariki baada ya kuangukiwa na mgodi ambao ulikuwa hautumiki nchini Ghana.
Maafisa wamesema kuwa kulikua na maporomoko ya ardhi katika sehemu ambayo ilikua haitumiki karibu na mji wa Kyekyewere ambao una sifa ya kuwa na wachimbaji haramu wa migodi.
Kwa mujibu wa maafisa wakuu, Waokoaji waliondoa miili 16 baada ya mgodi huo kuporomoka siku ya Jumatatu.
Haijulikani idadi ya watu waliokuwemo ndani ya mgodi huo , lakini imedaiwa kuwa hakuna dalili kuonyesha kuwa bado kuna miili mingine ndani ya mgodi huo.
Afisa mmoja ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mchimbaji mmoja aliyekuwa amejeruhiwa alifariki baadaye hospitalini. Hii inaongeza idadi ya waliofariki hadi 17.
No comments:
Post a Comment