HOME

Apr 22, 2013

HORACIO CARTES..RAIS MPYA WA PARAGUAY!!

Mfanyabiashara Horacio Cartes amechaguliwa kuwa rais wa Paraguay baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika jana nchini humo na kuonyesha kuwa chama cha Colorado kimeshinda uchaguzi huo.

Rais huyo mpya anakabiliwa na changamoto za kupambana na umaskini wa hali ya juu na kumaliza kutengwa kwa nchi hiyo kufuatia kitendo cha mwaka uliopita cha kutaka kumuondoa madarakani rais Lugo.

Mfanyabiashara huyo mwenye mafanikio na mdau wa soka, anamiliki zaidi ya makampuni 20 baadhi ya kujishughulisha na tumbaku, nyama na vinywaji, katika kampeni yake aliahidi mabadiliko ya usalama, elimu na afya.

No comments:

Post a Comment