Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. |
Wananchi wa Kenya watashiriki katika uteuzi wa baraza la mawaziri la serikali ya rais Uhuru Kenyatta orodha inayotarajiwa kutangazwa wiki hii.
Spika wa bunge Justin Muturi amethibitisha kuwa kamati ya bunge ya uteuzi itakusanya maoni kutoka kwa wananchi kuhusiana na wanaofaa kuwepo katika orodha hiyo ya baraza la mawaziri la Kenya.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Kenya kwa wananchi kupewa nafasi ya moja kwa moja kutoa mawazo yao na kushiriki katika uteuzi wa maafisa hao wa ngazi ya juu katika serikali ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment