HOME

Apr 25, 2013

WATCH: MAKALA YA NYUMA YA PAZIA YA SIRI YA MTUNGI!!

Siri ya Mtungi ni Tamthilia inayofurahisha ambayo msimu wake wa kwanza umemalizika kupitia uliokuwa ukirushwa Tanzania kupitia ITV kila Jumapili saa 3.30 Usiku na EATV kila Jumatano saa 3.30 usiku. Tamthilia hii ilikuwa ikionyesha maisha halisi ya watanzania ambapo ikawa kivutio kwa watu mbalimbali ambao walikuwa hawakosi kutazama.

Mpangilio mzima wa tamthilia ulikuwa kivutio lakini labda wengi wetu tulikuwa hatufahamu kilichojiri haswa wakati wa utengenezaji wake. Hii hapa ni makala maalum inayoonyesha nyuma ya Pazia ya utengenezwaji wa tamthilia hiyo ya Siri ya Mtungi. Ni Makala ya kusisimua ambayo watengenezaji wa Filamu Tanzania wanaweza kujifunza kitu haswa katika uongozaji wa filamu zenye ubora na viwango vya kimataifa. Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea tovuti yao. http://www.siriyamtungi.com/

No comments:

Post a Comment