HOME

Apr 19, 2013

CONFESSION: DIAMOND HAJAWAHI MEET NA BI KIDUDE!!

Msanii Diamond (katikati) akiwa na Fid Q na waombolezaji wengine wakimwombea dua marehemu Bi. Kidude nyumbani kwake jana (Picha na Jestina George
Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Diamond ambaye aliungana na mamia ya ndugu jamaa marafiki na wadau mbalimbali katika mazishi ya msanii mkongwe wa muziki wa Taarab Tanzania, Fatma binti Baraka, maarufu kama Bi Kidude huko Katumba Zanzibar, amekiri kuwa hajawahi kukutana na gwiji huyo.

Diamond pia ameeleza jinsi alivyoshtushwa na habari hiyo ya mshtuko kupitia kwa Dj Choka mbaya ambaye ndie wa kwanza kumhabarisha Diamond kwa kumpostia ujumbe wa kifo cha gwiji huyo mkongwe wa Taarabu nchini.

Kwa mujibu wa taarifa, Bi Kidude amefariki dunia kutokana na Ugonjwa wa Kisukari na vile vile uvimbe aliokuwa nao katika kongosho na anakadiriwa kufariki akiwa na umri wa zaidi ya miaka 100.

No comments:

Post a Comment