Onesmus Mwangi, 20, akiwa na maafisa usalama kijijini kwao, nyuma ni Helikopta aliyotengeneza na kusema yuko mbioni kuirusha. |
Kijana mmoja Onesmus Mwangi, 20, ambaye ametengeneza helikopta kwa kutumia vyuma chakavu na plastiki katika eneo la Githunguri, Kaunti ya Kiambu nchini Kenya ametahadharishwa dhidi ya kujaribu kuipaisha angani bila kibali cha wakuu wanaohusika.
Naibu wa kamishna wa polisi wa Githunguri, Bw Fredrick Ndunga amesema utaratibu unaostahili lazima ufuatwe kwa mtu yeyote anayejitokeza na ugunduzi wa kitu chochote.
Ndunga ameonya kuwa haitaruhusu watu kufanya majaribio hatari ambayo yanaweza kudhuru maisha ya watu.
Ndunga alitoa tahadhari hiyo afisini kwake jana baada ya kijana huyo kuwashangaza wakazi wa eneo hilo aliposema kuwa yuko karibu kuendesha ndege yake ambayo imemchukua miezi saba kutengeneza.
No comments:
Post a Comment