Zoezi la kuwatafuta waliofunikwa na kifusi linaendelea baada ya jengo kuanguka katika mji wa Bangladeshi, Dhaka na kusababisha vifo vya watu 147.
Wafanyakazi wa uokoaji wanafanya kazi kwa nguvu zote na watu wa kujitolea wakitumia vifaa na mikono kutafuta kuwaokoa waliosalimika kutokana na jengo hilo kuanguka.
Makumi kwa maelfu ya familia zilizopoteza ndugu zao walionekana katika eneo hilo wakiwalilia ndugu zao waliopoteza maisha.
Jeshi la polisi limesema kuwa wamiliki wa kiwanda hicho walidharau tahadhari ya kutowaruhusu wafanyakazi wao kuingia katika jengo hilo baada ya nyufa kugundulika siku ya Jumanne.
Matukio ya majengo kuporomoka nchini Bangladesh ni ya kawaida kutokana na majengo mengi marefu kujengwa kinyume na sheria za ujenzi.
Serikali ya nchi hiyo imetangaza siku moja ya maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoto kuwakumbuka waliopoteza maisha kufutia tukio hilo.
Picha: Reuters
No comments:
Post a Comment