HOME

Apr 22, 2013

MAMIA WAFA KATIKA MAPIGANO NIGERIA!!

Mapigano makali kati ya wapiganaji wa kiislamu na vikosi vya usalama Kaskazini mwa Nigeria yameripotiwa kusababisha vifo vya watu 185 na kuharibu nyumba 2000.

Maafisa wa serikali na jeshi wamesema kuwa wapiganaji walitumia silaha kali na roketi yenye mabomu mazito kupambana na vikosi vya jeshi karibu na mpaka wa nchi hiyo na Chad.

Nigeria inakabiliwa na hali ya hatari katika jimbo la kaskazini mwa nchi hiyo ambapo hali kama hiyo iliyoletwa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram na kusababisha vifo vya maelfu ya watu mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment