Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak ameamriwa kurejea gerezani kutoka katika hospitali ya kijeshi.
Mahakama ya rufaa jijini Cairo imesema kuwa kesi ya Mubarak itaanza kusikilizwa upya Mei 11 mwaka huu.
Mubarak anashtakiwa kwa pamoja na waziri wake wa zamani wa mambo ya ndani na maafisa sita wa usalama wakidaiwa kuhusika na mauaji ya mamia ya waandamanaji January mwaka 2011.
Awali kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa April 13 lakini ikaahirishwa baada ya mmoja wa majaji kujitoa kwenye kesi hiyo.
No comments:
Post a Comment