Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla imekumbwa na huzuni kubwa kufuatia taarifa za kifo cha aliyekuwa Seneta wa Jimbo la Makueni na mwanasheria maarufu Mutula Kilonzo aliyekutwa amekufa nyumbani kwake mapema siku ya Jumamosi.
Uchunguzi wa mwili wake unatarajiwa kufanyika leo pale Lee Funeral Home ambapo,
Mwili wa mwanasiasa huyo ulipelekwa katika nyumba hiyo kwa ajili ya kuhifadhiwa Jumamosi usiku baada ya kukutwa amefariki nyumbani kwake katika ranchi ya Maanzoni iliyopo kaunti ya Machakos.
Mwanasayansi mkuu wa elimu ya magonjwa (Mwanapatholojia), Dk. Johansen Oduor atafanya uchunguzi huo akishuhudiwa na wanafamilia wa marehemu Kilonzo na aliyekuwa daktari wake.
Matokeo ya uchunguzi huo yanatarajia kutolewa kesho ambapo taarifa za awali zinaonyesha kuwa hakukuwa na majeraha yoyote katika mwili wake.
Vyanzo vya habari vimesema kuwa kuna uwezakano Marehemu Kilonzo akazikwa siku ya Ijumaa wiki hii wakati uchunguzi wa kifo chake ukiendelea.
Kethi alikuwa na akiwakilisha upande taasisi isiyo ya kiserikali ya Africog na kufananishwa sana na baba yake kutokana na umahiri wake aliounyesha katika kesi hiyo.
Hii hapa ni taarifa ya Televisheni cha Citizen Kenya ikielezea zaidi kuhusiana na kifo cha Mheshimiwa Mutula Kilonzo.
No comments:
Post a Comment