HOME

Apr 25, 2013

MAKAMPUNI TANZANIA YAFUNDISHWA KUKABILI CYBER CRIME !!

Nchi za Afrika Mashariki zimetakiwa kuiga mfano wa Kenya kwa kutunga sheria itakayoshughulikia kesi zinazohusu makosa ya uhalifu yanayofanywa kwa njia ya mtandao.

Afisa kutoka asasi ya Cyber crime ambayo makao yake makuu barani Afrika yapo jijini Nairobi nchini Kenya, Bw. Sammy Kioko amesema hayo wakati wa mafunzo ya namna makampuni ya nchini yanavyoweza kudhibiti uhalifu kwa njia ya mtandao ikwemo wizi wa pesa katika mashine za kutolea fedha katika benki maarufu kama ATM.

Kioko amefafanua kuwa ukosefu wa sheria hiyo kunahatarisha juhudi za kujenga mtengamano imara wa Afrika Mashariki, hususani soko la pamoja la jumuiya hiyo ambalo kwa kiasi kikubwa malipo na taarifa zake muhimu zinasambazwa kwa njia ya mtandao.

Msikilize Bw. Kiondo akielezea zaidi suala hilo

No comments:

Post a Comment