HOME

Apr 19, 2013

MUSHARRAF AKAMATWA!!

Pervez Musharraf wa Pakistani.
Ripoti kutoka nchini nchini Pakistani zimesema kuwa polisi katika nchi hiyo wamemkamata rais wa zamani Pervez Musharraf na kumfikisha mahakamani.

Picha za televisheni zimeonyesha Musharraf akiwa na maafisa wa polisi waliokuwa wamevaa kiraia katika mahakama ya Islamabad.

Alhamis iliyopita mahakama nchini humo iliamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi kwa tuhuma za kutoa amri wakati akiwa madarakani ya kuzuiliwa kwa majaji mnamo wa mwezi Machi mwaka 2007.
.

No comments:

Post a Comment