Malkia Elizabeth wa Uingereza leo alikuwa miongoni mwa watu
mashuhuri waliohudhuria ibaada ya mazishi ya aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Uingereza Margaret Thatcher ibada iliyofanyika Kanisa kuu la mtakatifu Paul jijini London.
Wawakilishi 2300 kutoka mataifa 170 duniani waliwakilisha nchi zao
katika mazishi hayo kwa aliye kuwa waziri mkuu wa Uingereza
aliyekaa madarakani kwa kipindi kirefu na kufariki April 8.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amewaambia kusanyiko
lililokusanyika katika kanisa hilo kuwa mazishi wa kiongozi huyo
yameendana na jinsi ambavyo alijijengea heshima duniani kote.
Malkia wa Uingereza alikuwepo katika mazishi hayo |
Mjukuu wa Thatcher akisema machache kuhusu bibi yake mpendwa |
No comments:
Post a Comment