Majina ya wasanii wa muziki Tanzania ambao wameweza kuingia katika kinyang'anyiro cha tuzo za muziki za Kilimanjaro, yametangtazwa leo rasmi jijini Dar es Salaam ili kuanza mchakato wa kupata washindi wa tuzo hizo kwa mwaka huu wa 2013.
Katika mchakato wa mwaka huu na kama hatua moja ya maboresho yake, Vipengelea ambavyo vitakuwa vikishindaniwa mwaka huu vimeongezeka na kufikia 35.
Wasanii ambao wameweza kung'ara kwa kutokelezea katika vipengele vingi ni pamoja na Ommy Dimpoz ambaye anatokelezea mara 7 katika categories 6, Ben Pol ambaye anatokelezea mara 6 katika categories 7, Kala Jeremiah na Fid Q katika categories 4 na wengineo.Mkuu wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Angelo Luhala akizungumza machache katika zoezi la kutaja majina hayo.
Tuzo za Kilimanjaro Music zitafanyika kwa mwaka huu tarehe 8 Mwezi Juni katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na katika kipindi hiki cha kati hatua zitakazofuata ni pamoja na Semina kwa wasanii na Upigaji kura ambao utaanza Mei tarehe 2.
Tuzo hizo zimeletwa na kampuni ya bia ya Tanzania kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la sanaa Tanzania BASATA.
No comments:
Post a Comment