HOME

Apr 25, 2013

MALARIA BADO TISHIO DUNIANI!!

Wakati Jumuiya ya Kimataifa ikiwa inaadhimisha Siku ya Malaria Duniani ifikapo kila mwaka tarehe 25 Aprili, Malaria bado inawakilisha matatizo makubwa ya afya duniani huku nchi 99 zikiendelea kukabiliwa na maambukizi ya ugonjwa huo na watu zaidi ya 650,000 wakifariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa Malaria.

Tangu mwaka 2000 kiwango cha vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Malaria kimepungua kwa asilimia 25%. Kuna nchi 50 kati ya nchi 99 zinazoendelea kufanya vyema ili kufikia Malengo ya Maendeleo ya Millenia kwa mwaka 2015 kwa kupunguza vifo kwa asilimia 75%.

Malaria ni ugonjwa unaoendelea kupukutisha maisha ya watu wapatao 660,000 kutoka kila kona ya dunia, wengi wao ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanaoishi Kusini mwa Jangwa na Sahara.

Zaidi ya watu millioni 200 wanashambuliwa na ugonjwa wa Malaria. Kesi nyingi hazipimwi wala kupatiwa tiba muafaka. Dawa zisizo na viwango zinasababisha usugu, jambo ambalo linaweza kukwamisha jitihada za Jumuiya ya Kimataifa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria.

Kauli mbiu inayoongoza Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa Mwaka 2013; Wekeza kwa siku za baadaye. Shinda Malaria.

Credits: WHO, unmultimedia and AP

No comments:

Post a Comment