Familia ya mchezaji wa timu ya Bolton Fabrice Muamba ime post kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa Twitter picha ya mchezaji huyo akiwa amekaa katika chumba chake hospitalini.
Hiyo ni picha ya kwanza kutolewa hadharani tangu apate matatizo ya moyo katika mechi ya michuano ya kombe la FA kati ya timu yake na Tottenham Machi 17 mwaka huu.
Mchezaji
huyo mwenye miaka 23 alianguka uwanjani na kupata mshtuko wa moyo kabla ya kufikishwa hospitali ambapo kwa mujibu wa madaktari hali yake inaendlea vizuri sana kulinganisha na awali alivyofikishwa hospitalini hapo.
No comments:
Post a Comment