HOME

Mar 7, 2012

UHABA WA DAWA WAZIKUMBA HOSPITALI CONGO BRAZAVILLE!!


Kuna uhaba wa mkubwa wa dawa huko nchini Congo Brazaville wakati hospitali zinaendelea kuwapatia matibabu zaidi ya watu 1300 waliojeruhiwa kutokana na milipuko kutoka ghala la silaha uliotokea nchini humo jumapili iliyopita.


Mamia ya majeruhi wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya chuo kikuu ambapo majeruhi hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika viambaza na mahema ambayo yamejengwa katika eneo hilo.


Habari zinasema pamoja na baadhi wa majeruhi kupewa cheti cha dawa lakini dawa zimekwisha katika maduka yanayouza dawa ikiwa ni pamoja na maduka binafsi.

No comments:

Post a Comment