Naibu waziri wa Nishati na madini Mhe. Adam Kigoma Malima akiwaelezea waandishi wa habari (Hawapo Pichani) jinsi alivyoibiwa nje ya hoteli hiyo ya Nashera mkoani Morogoro. |
Naibu waziri wa nishati na madini nchini Tanzania Adamu Kigoma Malima ameibiwa mali zake zikiwemo nyaraka muhimu,hati za kusafiria na fedha taslimu zikiwemo dola za kimarekani elfu 4000 na shilingi milioni 1.5 za kitanzania kwenye hoteli ya kitalii ya Nashera Mjini Morogoro alikokuwa amefikia.
Mhe. Malima amefanyiwa uhalifu huo katika hoteli hiyo aliyokuwa amefikia kwa takribani siku tatu akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani humo, ambapo waandishi wa habari baada ya kupata taarifa hizo, walikwenda katika hoteli hiyo na kuonana na uongozi.
Hata hivyo mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Morogoro Hamis Suleiman, alipohojiwa amekiri naibu waziri huyo kugundua wizi huo majira ya saa 10.45 alfariji, mnamo machi 09 mwaka huu, ambapo mali zilizoibwa ni pamoja na dola za Marekani elfu 4000, shilingi milioni 1.5, pete mbili za silva zenye thamani ya shilingi milioni 2, simu tatu za mkononi zenye thamani ya shilingi milioni 1.3, balaghashia yenye thamani ya shilingi 50,000, kompyuta mbili za mkononi zenye thamani ya shilingi milioni 5.6, tape recorder na headphone zake zenye thamani ya shilingi milioni moja.
No comments:
Post a Comment