Mar 1, 2012
WANAFUNZI 18 WAMEKULA SUMU YA PANYA WAKIDHANI ''GLUCOSE''!!
Wanafunzi 18 wa shule ya msingi Namirembe ambayo ni ya bweni nchini Uganda Mashariki mwa wilaya ya Budaka wamekimbizwa katika kituo cha afya cha Budaka baada ya kula sumu ya panya wakidhani Glucose.
Kwa mujibu wa makamu mkuu wa shule hiyo Robert Mukasa mwanafunzi Cryspus Looki siku ya Jumanne alibeba sumu ya panya kutoka nyumbani kwa bibi yake ambaye anaishi nae.
Amesema idadi hiyo ingeweza kuwa kubwa zaidi lakini kilichowaokoa wanafunzi wengine ni mvulana mmoja ambaye aliiona box likiwa na lebo ya panya na kuwataarifu walimu kuwa rafiki zake wamekula sumu ya panya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment