HOME

Mar 1, 2012

HOSPITALI ZA MULAGO, AAR MAHAKAMANI KUFUATIA KIFO CHA MKE WA MBUNGE!!


Maafisa wa Hospitali ya Mulago nchini Uganda ikiwa ni pamoja na maafisa wa huduma ya afya ya  AAR Health Services leo wamefikishwa mahakamani kujitetea kufuatia kesi ya madai ya kusababisha kifo cha mke wa mbunge Benard Mulengani kutokana na uzembe.


Mulengani amezishitaki hospitali hizo kufuatia kifo cha mke wake, Gloria Kyasimire,ambaye alikufa February 7, 2010 baada ya kushindwa kulinganisha damu baada ya kupatiwa damu ya group B+,wakati marehemu kundi lake la damu lilikuwa O+.


Mbunge huyo wa bunge la Afrika mashariki alifungua madai hayo katika mahakama kuu ya nchi hiyo na anataka kulipwa fidia ya shillingi millioni 542.

No comments:

Post a Comment