Mar 19, 2012
UNICEF KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA!!
Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto (UNISEF) limeahidi kuendelea kuisadia Tanzania kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa hapa nchini .
Hayo yamesemwa na baadhi ya wawakilishi kutoka shirika hilo ambao waliotembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na shirika hilo katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Hai DR. Norman Sigala amesema miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano na shirika hilo imeiwezesha wilaya hiyo kupunguza matatizo mengi likiwemo la vifo vya akina mama na watoto na pia maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Hai ni miongoni mwa wilaya zilizobahatika kuwa na miradi inayofadhiliwa na shirika hilo ambayo pia imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa unaohitaji kuigwa na wilaya zingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment