Mar 19, 2012
MJADALA WA TAREHE YA UCHAGUZI KENYA WAONGEZEKA!!
Asasi ya kiraia nchini Kenya (NCSC) imewataka wakuu wawili wa nchi rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga kuvunja serikali ya muungano ifikapo Oktoba 19 mwaka huu ili kuruhusu wanannchi kufanya uchaguzi mkuu mwezi huo kama inavyopendekezwa na watu wengi.
Akizungumza jijini Nairobi siku ya Jumapili rais wa asasi hiyo Morris Odhiambo amesema tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC) imetoa siku ya kufanyika uchaguzi huo kuwa Jumamosi na si tarehe ya mwisho.
Nae mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto ametoa kauli kama hiyo akisema kikomo cha muhula wa pili wa urais ni Disemba 31 mwaka huu wakati muhula wa bunge unamalizika Januari 5 mwakani vinginevyo itakuwa ni kinyume cha katiba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment