HOME

Mar 28, 2012

BESIGYE ASHTAKIWA!!

Kiongozi wa upinzani Dk. Kizza Besigye na wengine 14 wameshtakiwa mahakamani kwa kosa la kufanya mkutano kinyume cha sheria ambao ulisababisha kutoa mauaji ya naibu inspekta wa polisi (AIP)  John Bosco Ariong.


Besigye pamoja na Bw. Lukwago,Meya wa wialaya ya Kawempwe Bw. Mubarak Munyagwa,kiongozi wa wanawake wa chama cha FDC Ingrid Turinawe na mbunge wa wanawake wa jiji la Kampala Nabilah Naggayi na Mwanaharakati wa haki za wanawake  Catherine Dembe leo walisimama mbele ya hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya Buganda Road Eleanor Khainza.


Mashtaka hayo pia yanahusisha kumjeruhi askari aliyekuwa zamu ambapo mwanasheria wa watuhumiwa hao David Mpanga aliwasilisha mahakamani kuwa watuhumiwa hao ni wanajamii wanaoheshimiwa.

No comments:

Post a Comment