HOME

Mar 6, 2012

WAANDISHI WA HABARI MKOANI IRINGA WAANDAMANA KUPINGA UNYANYASAJI DHIDI YAO!!


Waandishi wa habari mkoani Iringa wameandamana kupinga vitendo vya  unyanyasaji na urasimu wa habari vinavyofanyiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa iringa na idara zake huku mkuu wa mkoa huo akikataa kupokea maandamano hayo.


Maandamano hayo yaliyoanzia katika viunga vya bustani ya manispaa ya Iringa na kupitia katika barabara ya Uhindini,Mshindo ,Mashine tatu na kurudi katiaka barabara ya Uhuru yalihitimishwa katika viunga hivyohivyo vya manispaa.


Nao baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki maandano hayo wamelishukuru jeshi la polisi mkoani humo kwakutoa kibali na kulinda maandamano hayo hali iliyofanikisha kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa kama walivyoona inafaa huku wakimshangaa mkuu wa mkoa huu Christine Ishengoma kukataa kuyapokea licha yakuhakikishiwa  kuwa ni maandamano ya amani.

No comments:

Post a Comment