HOME

Mar 19, 2012

WADAU MBALIMBALI WA SOKA DUNIANI NA WACHEZAJI WAENDELEA KUMUOMBEA FABRICE MUAMBA!!

 Mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba dakika chache kabla ya kuanguka uwanjani siku ya Jumamosi

Cahill akionyesha shirt yake aliyovaa ndani ya jezi yake ya Chelsea kuonyesha sapoti yake kwa Muamba ambaye yuko mahututi hospitalini

Wachezaji,mameneja na wadau wa soka barani Ulaya wameonyesha kumuunga mkono mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba ambaye yuko mahututi baada ya kuanguka akiwa uwanjani siku ya Jumamosi wakati wa mechi kati ya timu yake ya Bolton Wanderes na Tottenham Hotspurs.


Mchezaji huyo wa kiungo alipatwa na shambulio la moyo wakati wa mchezo dhidi ya Tottenham kombe la FA, na inasemekana iliwachukua madaktari takribani masaa mawili kuuchochea moyo wa mchezaji huyo ambaye bado yuko katika uangalizi wa madaktari.


Taarifa za mwisho kutolewa zinadai kwamba bado mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yuko kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Meneja wa Bolton Wanderers, Owen Coyle, alisema anatumaini matokeo yatakuwa mema kwa Fabrice Muamba, huku mchezaji huyo akiwa anaendelea kuuguzwa.

Coyle amesema hayo nje ya London Chest Hospital, ambako ndiko Fabrice anakotibiwa baada ya kuzirai wakati Bolton Wanderers wanacheza na Tottenham Hotspur kwenye uwanja wa White Hart Lane saa 12 magharibi.


 

No comments:

Post a Comment