HOME

Mar 23, 2012

AFANDE SELE AWACHANA VINEGA...AIFANANISHA BONGO FLEVA NA SHAMBA AMBALO SASA LIMEISHA RUTUBA!!

Mkali wa Rymes Afande Sele akiwa na Fadhili Kiwia kutoka dawati la Enews ya EATV na Michael Lukindo kutoka The Requeast Show ya East Africa Radio.

Afande Sele pamoja na Zembwela kutoka Super mix ya East Africa Radio.

Afande Sele akiwa na Michael Baruti (kushoto) na Zembwela (Kulia)

Afande Sele pamoja na Music Coordinator wa East Africa Radio Big Man Kim ''DJ KIM''

Mkali wa Rymes msanii wa Bongo Fleva Dume la Simba Afande Sele amefunguka mengi kuhusu muziki kwa ujumla baada ya kimya cha muda mrefu wakati akizungumza na blog hii leo pamoja na shutuma mbalimbali alizopata kuwa yeye ni msaliti wa kundi la Vinega na kudai kuwa yeye na Mh. Joseph Mbilinyi ''Sugu'' ndio waanzalishi wa kundi hilo lakini ''Mchwa'' ants wa kundi hilo ndio wanafiki kwa kuwa wamefanya mengi ikiwemo kumnyima shoo zilizokuwa zikiandaliwa na kundi hilo katika mikoa mbalimbali kama Mbeya na lile la Uzinduzi wa Albam ya Anti Virus lililofanyika katika viwanja vya Ustawi wa jamii hivi Karibuni.


Amemshushia shutuma Soggy Doggy na kusema anamshangaa jinsi alivyo ni mtu wa ajabu na anahitaji kuombewa kwani ni mnafiki na yeye ndio chanzo cha yote haeleweki''.

Afande amesema yeye ni mfalme na kamwe hawezi kuishiwa pamoja na maneno ya shutuma nyingi juu yake za kufeli na kupotea katika Game na hata kuwa anambania Dogo Ditto wakati ni mdogo wake na sasa anafurahia mafanikio na matunda ya Ditto.


Afande Sele pia amefunguka kushusu muziki wa Bongo Fleva ambapo amesema na kusema muziki huo ambao ni shamba sasa limeisha rutuba kwani yamebaki makapi mwanamuziki wa mwisho kuzalishwa kwenye shamba hilo ni Fid Q wanaofuata hawajui nini wanafanya na kuwaita ''Maua Saa sita''


Sele amesema ''Mwanamuziki ni sawa na ua ndani ya bustani kubwa ya Muziki, kazi kwako kuchagua unataka uwe ua la aina gani!! MauaSaaSita Mjipange''

No comments:

Post a Comment