HOME

Mar 27, 2012

KENYA YAGUNDUA MAFUTA TURKANA!!

Kenya imegundua hazina ya kwanza ya mafuta katika kile kinaachoonekana kuwa ni mafanikio makubwa katika shughuli za utafutaji mafuta na gesi nchini humo.


Mafuta hayo yamegunduliwa katika eneo la Turkana na kampuni ya utafutaji mafuta kutoka nchini Uingereza ya Tullow Oil ambayo ndio iligundua mafuta katika bonde la Albertine magharibi mwa Uganda na nchini Ghana.


Akitangaza habari za kupatikana kwa mafuta, rais Mwai Kibaki amesema mafuta hayo yamepatikana katika kisima cha Ngamia kilichopo kijiji cha Kodekode wilaya ya Turkana Mashariki, umbali wa mita elfu moja chini ya ardhi.

No comments:

Post a Comment