Mar 1, 2012
MADIWANI WAWANG'OA WABADHIRIFU MONDULI!!
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya monduli Mkoani Arusha limewafukuza kazi wakuu watano wa idara katika halmashauri hiyo na kumpa likizo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo baada ya kubainika kwamba wamesababisha ubadhilifu mkubwa wa fedha wa zaidi ya shilingi milioni mia tatu kwenye miradi mbalimbali
Uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha dharura kilichoitishwa na mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo kufuatilia hatua zilizochukuliwa kwa wakuu hao wa idara
Wakuu hao ni pamoja na mkuu wa idara ya uhandisi mhandisi Silvester Chinengo,mkuu wa usafirishaji Bw Rajab Jabu,mkuu wa manunnuzi na ugavi Bw Kilango Mwangwala,Mweka hazina Julius Mollel na mhasibu Nico Mchicha huku mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bw Samwel Mlay akipewa likizo
Madiwani Julius Kalanga ,Isaack Copriano na Gideon Shoo katika kikao hicho wame itaka wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa, TAMISEMI kuridhia maamuzi hayo kwa madai ya kwamba tuhuma zinazowakabili ni kubwa zikiwemo za kutoa zabuni hewa na kusababisha kazi kufanyika chini ya kiwango
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment