HOME

Mar 15, 2012

WAUGUZI WASITISHA MGOMO NCHINI KENYA!!


Mgomo wa wiki mbili wa wauguzi na wafanyakazi wengine wa sekta ya afya nchini Kenya jana umemalizika rasmi kufuatia mkutano kati ya viongozi wa vyama na waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga.


Kufuatia mfumo wa rejea kazini barua zote za kufukuzwa kazi kwa wauguzi hao waliogoma zilifutwa ambapo katika taarifa iliyosomwa na naibu waziri katika ofisi ya waziri mkuu Bw. Alfred Khangati wafanyakazi hao wamehakikishiwa kutonyanyaswa.


Hata hivyo Bw. Khangati amesema wafanyakazi wa sekta ya afya watakaoshindwa kuripoti katika majukumu yao hadi leo watachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria zilizopo za utumishi wa umma.

No comments:

Post a Comment