Mar 26, 2012
''THE HUNGER GAMES'' YATENGENEZA REKODI US BOX OFFICE!!
Filamu mpya ya ''The Hunger Games'' imeshika nafasi ya juu kabisa ya U.S. box office kwa kuvunja rekodi ya kuingiza kipato kikubwa katika siku ya kwanza ya kuachiwa kwake ikishuudia kuingiza dola milioni 155.
Filamu hii kali kuwahi kutokea pamoja na wahusika wake Jennifer Lawrence, Liam Hemsworth na Josh Hutcherson wamejipatia umaarufu mkubwa katika siku za karibuni tangu kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kwa kazi yao huko Marekani.
Hunger Games sasa inakuwa filamu ya tatu kushikilia rekodi ya ufunguzi mzuri na wa mafanikio kuliko zote nyuma ya Harry Potter mwaka jana na The Deathly Hallows: Part 2 ya mwaka 2008 ambazo zote pia zilijivunia mamilioni ya dola katika mauzo yake ya siku ya kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment