HOME

Mar 12, 2012

NCHI HAIWEZI KURUDI TENA GIZANI-MHE. JANUARY MAKAMBA!!

Mhe. January Makamba (katikati) akiwa na watangazaji wa kipindi cha Supermic cha East Africa Radio Michael Baruti (kushoto) na Zembwela (kulia) leo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Tanzania, Mh. January Makamba amesema kamati yake imejipanga kuhakikisha kuwa taifa haliingi gizani tena kama ilivyokuwa hapo nyuma.


Akiongea leo kwenye kipindi cha Supa Mix cha East Africa Radio Mh. Makamba amesema kamati yake inayoendeshwa na yeye ambae ni kijana kamwe haitorubuniwa na kuingia katika mitego ya kununuliwa na makampuni ya kigeni.


Mheshimiwa Makamba pia amezungumzia suala la kuwezesha vijana kupata elimu ya nishati ya mafuta na gesi ambapo kamati yake imetoa maelekezo kwa TPDC kutumia fedha za mafunzo zipatazo dola milioni 1.8 zinazotolewa kila mwaka na makampuni ya mafuta na gesi kusomesha vijana.

1 comment:

  1. KAZI SAFI SANA MNAFANYA MICHAEL NA MZEE WANGU ZEMBWELA KUTOKA MIKOCHENI NAPENDA SANA SUPA MIX NIKIWA MAENEO YA 94.7 NAIROBI.NA PIA MREMBO MARYGORETHI RICHARD SHIKILIA UZI HUO HUO KWA USOMAJI HABARI UKO JUU TU SANA KAMA MAWINGU.

    ReplyDelete